Je naweza kucancel order na kupata refund?

NDIO

Pesa yako inapoingia katika account yetu nakuhakikishia iko katika mikono salama.Unaweza ukacancel order muda wowote kabla mzigo wako haujafungwa, kabla order nzima haijamalizwa kulipwa. Endapo ukacancel order, utalazimika kulipa makato yafuatayo kwenda CRDB ni 1000tsh kwenda banks nyingine ni 1500tsh
Endapo Bidhaa za zee ika cancel order yako kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu MTEJA HAKATWI PESA YOYOTE KUFANYA REFUND

Je naweza kuagiza Simu na nyinyi?

HAPANA

Hapana! Kwa bahati mbaya biashara yetu kwa sasa haijihusishi na uuzaji wala usambazaji wa vifaa vya electronics ikiwemo Simu, Saa, Laptop na Games.

Process zenu za kuagiza zikoje?

PROCESS

Bidhaa za Zee tunapokea order kwa mfumo ufuatao: Mteja anaeka order kwa muundo wa list mfano:
1) chupi dozen 100
2) gauni piece 150
Order ikishakamilika ndipo malipo yanapoanza. Hatupendelei kufunga order nusu. Bila invoice kutolewa HATUPOKEI PESA.
Baada ya order kulipwa, ndani ya siku10 mzigo unakuwa umefungwa na kuanza safari. Kisha unasubiri kupigiwa simu kulipia usafiri na kupokea mzigo wako. Mzigo unachukua sio chini ya siku 45 mpaka kukufikia Tanzania.
MIZIGO YOTE HUFIKIA DAR ES SALAAM KAGUA NA HESABU MZIGO WAKO OFISINI AU WAREHOUSE KABLA HAUJAONDOKA NAO

Je order inachukua mda gani tokea nimeeka order mpaka kuupokea Tanzania?

ORDER TIME

Order yoyote inachukua siku 5 hadi siku 10 kupangwa, kukaguliwa na kupelekwa warehouse ukiwa china. Njiani sio chini ya siku 45. Na ukishafika Tanzania mzigo kushushwa utachukua kuanzia siku 10 mpaka siku 20 uwe tayari kufatwa na mteja.

Je bei hizi za bidhaa ni pamoja na gharama za usafiri?

USAFIRI?

Hapana. Bei za Bidhaa zetu zote hazijajumlisha gharama za usafiri. Mteja ndiye anayelipia gharama za usafiri baada ya mzigo wake kufika Tanzania.

Kwa bahati mbaya gharama za usafiri wa mzigo wako ni mpaka mzigo upimwe. Hatuwezi Kukisia.

Unaweza kupata gharama za usafiri wa mzigo wako kupitia hii link

Track Your Shipment

Mnasafirisha mizigo yenu kutumia kampuni gani za usafirishaji?

COURIER

Kampuni za usafirishaji tunazotumia kutuma mizigo yetu ni:
Kwa ndege: TARGET EXPRESS
Kwa maji: TOSH LOGISTICS na BLUE WAVE CARGO.


Mteja anayeagiza full order(yani sio ya kuchanga) anayonafasi ya kuchagua kampuni aipendayo kusafirisha mzigo wake.

Track Mzigo Wako

Mzigo wangu ukishafika napataje taarifa?

DELIVERY

Mzigo ukifika huwa cha kwanza unapata msg au unapigiwa simu. Ukishapokea ujumbe huo wanakuelekeza ofisini uende ukalipie gharama za usafiri.

Endapo utahisi gharama za usafiri ziko juu usisite kuwasiliana na sisi tuweze kutafuta suluhisho.

Ukishafika ofisi za Tosh logistics unalipia gharama husika kisha unaenda kufata mzigo kwenye warehouses zilizoko mbozi jijini dar es salaam.

Bahati mbaya ofisi yetu hatutoi mizigo ya wateja godown unless kuwe na tatizo kubwa sana.

Kwa wateja wa mikoani ambao hawana watu wakuwachukulia mizigo yao usisite kuwasiliana na sisi tuweze kukusaidia

KUMBUKA

KAGUA MZIGO WAKO KABLA HAUJAONDOKA NAO GODOWN. HAKIKISHA JINA, NAMBA YA SIMU NA VITU ULIVYOAGIZA VYOTE VIKO SAWA.